T A N Z I A
Rais
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Tarsicius
Ngalalekumtwa, anasikitika kutangaza kifo cha Mhashamu Askofu Mstaafu Amedeus
Msarikie, wa Jimbo Katoliki Moshi, kilichotokea alfajiri ya leo saa 10.30 katika
hospitali ya Nairobi.
Habari
ziwafikie Maaskofu Wakatoliki wote Tanzania, Mapadre, Watawa, walei wote, ndugu,
jamaa na marafiki. Mipango ya Mazishi
inafanywa.
Marehemu Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie alizaliwa
katika kijiji cha Makunduchi Kirua Vunjo katika Mkoa wa Kilimanjaro mwaka 1931,
alipata Daraja Takatifu la Upadri tarehe 08 Agosti, 1961 na akateuliwa na Baba
Mtakatifu Yohane Paul II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi tarehe 04 April,
1986. Aliwekwa Wakfu kuwa Askofu wa Moshi
tarehe 01 Mei, 1986 Jimboni Moshi.
Alistaafu rasmi kama Askofu wa Moshi kwa mujibu wa sheria za Kanisa
mwaka 2007.
Amefariki dunia leo tarehe 07 Februari, 2013
akiwa na umri wa miaka 82 ya kuzaliwa, 52 ya Upadri na 27 ya Uaskofu.
Via Mtandao-net TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment