Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika facebook ya NECTA,  huenda matokeo ya kidato cha nne yakatoka leo. Hata hivyo Mtandao huo ulisema kwamba kutoka kwa matokeo haya kutategemea kufanikiwa kwa mipango ya Baraza hilo. 
"Mambo yakienda vizuri kama tulivyopanga, matokeo tutayatoa kesho. Kwa kudokezea ni kwamba wasichana wameng'ara sana kwenye mitihani ya mwaka 2012.
Tuombe Mungu kila kitu kiende kama tulivyopanga."
Ilisema NECTA katika facebook yake jana. 

Tutazidi kuwapa taarifa zaidi.
Chanzo: necta.fb page TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top