Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza watendaji wote
kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuwapatia raia wa Tanzania
vitambulisho vinavyowahusu huku akiongeza kama watakiuka sheria na taratibu
watavuruga zoezi kuna hatari ya watu wasio raia kuvipata vitambulisho
visivyowahusu.
Mheshimiwa Rais amesema kwa wale watakaobainika
kutoa taaarifa za upotoshi kwa lengo la kuficha ukweli kwa makusudi hatua
stahiki za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Akizindua mfumo wa utambuzi na usajili vitambulisho vya
Taifa jijini Dar es Salaam Rais Kikwete amewataka Watanzania kushirikiana na
mamlaka ya vitambulisho ya Taifa NIDA kwa maendeleo ya Taifa.
Rais Kikwete amesema watanzania wanatakiwa
kujitokeza na kutoa taarifa sahihi ili kufanikisha zoezi la uandikishaji na
uhakiki wa taarifa za watu wote ili kufikia mwaka 2015 watanzania wote wapate
vitambulisho hivyo.
Rais Kikwete amesema ukosefu wa fedha kuwa
changamoto kubwa katika zoezi la utengenezaji wa vitambulisho vya Taifa ni
gharama kubwa hivyo serikali inafanya jitihada
za makusudi kuhakikisha watu wote wanakuwa na vitambulisho hivyo kwa kuvigharamia
Rais amesema kama serikali itajitahidi kutoa
ushirikiano kwa mamlaka ya vitambulisho ya Taifa NIDA kuhakikisha inaondoa na
kupunguza changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo ikiwemo upungufu wa rasilimali
watu na uhaba wa fedha.
Dakta Kikwete amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Watanzania watumie vitambulisho hivyo wakati wa
uchaguzi huo.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dakta Emmanuel
Nchimbi amesema tayari NIDA imeshampata mkandarasi na vituo vya kutunzia taarifa za elektroniki na kupata michoro ya ujenzi wa ofisi za
wilaya.
Akiongea katika uzinduzi
wa mradi huo mkurugenzi mkuu wa nida Bwana Dickson Maimu amesema kuna changamoto kubwa ya fedha na
rasilimali watu hivyo kumuomba Rais kuisadia mamlaka yake kulifanyia ufumbuzi
suala hilo.
0 comments:
Post a Comment