Hizi ni sura tofauti za kuharibika kwa gari ndogo aina ya Nissan iliyopata ajali eneo la Imezu Nje kidogo ya jiji la Mbeya jana tarehe 12/02/2013 saa 6.50 mchana. Ndani mna mwili wa dereva wa gari hii akiwa ameshakata roho.
Hapa ndipo lori kubwa lililogongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Nissan lilipoibania gari ndogo kabla ya lori hilo kupata upenyo na kupita.
Hili ni lori lenye namba T 573 APW lililogongana na gari ndogo aina ya Nissan eneo la Itezi Nje kidogo ya Jiji la Mbeya jan tarehe 12/02/2013 na kusababisha kifo cha dereva wa gari ndogo ya IT papo hapo.
Nyuma ni basi la Super Feo lililokuwa likitokea Songea kuelekea Mbeya likifuatiwa na Tiper aina ya Fuso na kisha Lori kubwa mbele ambayo dereva wa gari ndogo (sasa ni marehemu) alitaka kuyapita katika kimlima kilichopo eneo la Imezu nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Askari polisi akigawa gloves kwa waokoaji kwa usalama zaidi.
Hapa kiwiliwili cha Marehemu kimetolewa nje ya gari lakini miguu bado imenasa na jitihada za kumwondoa marehemu kwenye gari alilopata nalo ajali zikiendelea.
Mashuhuda wakiangalia kinachoendelea wakati zoezi la kuutoa mwili wa marehemu likiendelea. Lori linaloonekana lilikuwa limeharibika eneo hilo na ndipo gari zilipogongania.
Gari la zimamoto likiwasili eneo la tukio kwa uokoaji na kisha wakafunga mashine zao kukata vitu vilivyokuwa vimembana dereva wa gari ndogo iliyopata ajali.
Kikosi cha zimamoto kwa kushirikiana na polisi na raia wengine wakiwa kazini kuutoa mwili wa marehemu.
Mwili wa marehemu tayari umeshatolewa kwenye gari ndogo iliyopata ajali |
m |
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari la polisi tayari kupelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya. |
Kufa kufaana, jamaa wakijipatia mafuta kutoka katika tenki la mafuta lililong'oka kutoka kwenye lori lililogongana uso kwa uso na gari ndogo.
Hapa kikosi cha polisi kikiwahoji baadhi ya watu waliodaiwa kuhusika kumimina mafuta kutoka kwenye tenki lililong'oka kwenye lori lililogongana na gari ndogo.
Ajali ilitokea eneo la Imezu nje kidogo ya jiji la Mbeya jana tarehe 12/02/2013 majira saa 6.50 mchana ikihusisha gari ndogo aina ya Nissan (IT) iliyokuwa ikitokea Dar es Saalam kuelekea Tunduna ikiendeshwa na dereva ambaye jina lake halikufahamika mara moja iliyogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea mkoa wa Njombe.
Chanzo cha ajali ni dereva wa gari ndogo kutaka kuyapita magari matatu makubwa katika mwinuko na kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likishuka kutokea Mbeya kuelekea barabara ya mkoa wa Njombe na kusababisha kifo cha dereva wa gari ndogo papo hapo.
Chanzo cha ajali ni dereva wa gari ndogo kutaka kuyapita magari matatu makubwa katika mwinuko na kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likishuka kutokea Mbeya kuelekea barabara ya mkoa wa Njombe na kusababisha kifo cha dereva wa gari ndogo papo hapo.
Mwanabog akiwa katika basi la Super Feo lililopitwa na gari ndogo ya IT, alishuhudia dereva wa Super Feo akitaka kulipita gari lililokuwa limebeba tofali na lori lililokuwa mbele ya Fuso ghafla alirudi upande wake baada ya kupewa ishara na kondakta kuwa kuna gari linakuja mbele.
Aidha, shuhuda aliyekuwa amekaa jirani na dereva wa Super Feo aliongeza kuwa wakati basi linarudi kushoto kumbe dereva wa IT aliamua kulipita basi kwa kasi na kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linashuka.
Aidha mwanablog alishudia lori likiyumba baada ya kugongana uso kwa uso na gari ndogo hali iliyosababisha hofu ya kuligonga basi la Super Feo kwa vile lori hilo lilikuwa linakuja mbele likiwa linayumbayumba kwa kukosa mwelekeo.
Baada ya kuigonga gari ndogo, lori hilo lilipinduka jirani kidogo na eneo la ajali ya kugongana uso kwa uso.
Shuhuda mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake alisema kuwa lori lilipopinduka alimwona dereva wa lori hilo akitoka na kisha kukimbia kutoka eneo la tukio.
Lori lililogongana uso kwa uso lilidondosha tenki la mafuta ambayo yalianza kumwagika katika eneo hilo jambo lililowashawishi baadhi ya watu kuanza kuya chota. Mwanablog aliwasikia wakisema "hawawezi kutufanya kitu kwa vile mafuta yanamwagika na hawawezi kuyakinga tena". Walisema wachota mafuta bila kujua kwamba polisi wakiwa wanakuja kwa mbali walikuwa wanawaona wakichukua mafuta hayo.
Polisi walijitahidi kufika kwa wakati mwafaka ingawa changamoto kubwa ikawa ukosefu wa zana za kutumia kuutoa mwili wa marehemu ulionasa kwenye gari ndogo iliyokuwa imefinyangwa.
Bahati nzuri Mwili ulitolewa kwenye saa 7.45 baada ya kikosi cha zimamoto kufika na zana za kukatia vitu mbalimbali.
Bahati nzuri Mwili ulitolewa kwenye saa 7.45 baada ya kikosi cha zimamoto kufika na zana za kukatia vitu mbalimbali.
Mwili wa marehemu ambaye jina lake halikufahamika mara moja umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya.
PICHA ZOTE NA AZIMIO LETU BLOG
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment