Jeshi la polisi Mkoa wa Kinondoni linawashikilia
watuhumiwa 7 kwa tuhuma za kuingia nchini isivyo halali, kuwapokea na kuwahifadhi
raia wa kigeni isivyo halali na kujihusisha na biashara ya usafirishaji haramu wa
binadamu[Human Trafficking].
Kamanda wa polisi mkoa huo Charles Kenyela amesema tukio
hilo limetokea huko kimara Bonyokwa nyumbani kwa ISSA OMARY, kufuatia taarifa toka kwa wasiri wa
polisi zilizoelezea kwamba raia wa kigeni wasiofahamika walikuwa wamehifadhiwa
katika makazi yake.
Amesema Jeshi la
Polisi lilipofuatilia taarifa hizo kwa
kufanya upekuzi nyumbani kwake, mtuhumiwa huyo alitoroka na mara baada ya
upekuzi watu wanne[4]raia wa ETHIOPIA
walipatikana wakiwa wamefungiwa kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba hiyo
Katika mahojiana ya awali, watuhumiwa hao walieleza kwamba walitokea
nchini Ethiopia kupitia mpaka wa Tanzania hadi Dar es salaam ambako
wangesafirishwa kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Mtwara.
Kamanda Kenyela ameongeza kuwa siku moja baada ya kukamatwa
kwa wahamiaji hao, jeshi la polisi lilifanikiwa kumnasa mmiliki wa nyumba hiyo
na kuwataja wafanyabiashara wawili raia wa Burundi kuwa ndio wanaofanya
biashara hiyo
Watuhumiwa hao wawili pia walikamatwa kwenye hoteli ya Luch
Time Manzese jijini na kwamba taratibu za kuwafikisha mahakami zinafanyika
0 comments:
Post a Comment