Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za UKIMWI, AJAAT, Adolf Simon Kivamwo akizungumza jambo
Waandishi wa habari wametakiwa kuandika habari za ugonjwa wa UKIMWI kwa kufuata misingi ya weledi ili kupiga vita unyanyapaa unaoendelea kwa watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo. Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za UKIMWI, AJAAT Bwana Adolf Simon Kivamwo amewataka wanahabari kutambua kuwa mchango wao kwa jamii ni kuhabarisha,kuelimisha na kuonya jamii.

Mwenyekiti huyo amewataka  waandishi kuelimisha juu ya masuala mbalimbali kama unyanyapaa, suala ambalo limekuwa likirudisha nyuma jitihada za mapambano  dhidi ya UKIMWI katika jamii. Hata hivyo Bwana Kivamwo ametoa angalizo kwa waandishi kuhakikisha wanaripoti kwa usahihi na kuacha kutumia lugha inayowakatisha tama watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo

AJAAT ilianzishwa mwaka 2004 ambapo imekuwa ikiwezesha mafunzo kwa wanahabari na jamii kwa ujumla kupitia semina,warsha na machapisho
mbalimbali.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top