Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA limeagiza madereva wote hapa nchini kubadilisha leseni wanazotumia na kuanza kutumia leseni za kisasa ili kuendana na teknolojia iliyopo.

Afisa mnadhimu wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani Johansen Kanatano amesema madhumuni ya mfumo mpya wa leseni ni kudhibiti ongezeko la ajali, kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali na kubaini
leseni za kughushi kwa urahisi zaidi.

Afisa huyo amesema serikali ilishatoa utaratibu kwa madereva wote kubadili leseni hata kama hazijakwisha muda wake,ambapo mwisho wa kutumika kwa leseni za sasa utakuwa Machi 31 mwaka huu. Bwana Kanatano amesema mpaka kufikia Desemba 31 mwaka 2012 jumla ya leseni LAKI SITA NA ELFU 16 TU zilizotolewa, lakini TRA ina kumbukumbu ya vyombo vya moto milioni moja, laki moja  na elfu 64 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwa kuna madereva wanaendesha magari bila ya leseni.

Naye Kamishina msaidizi wa TRA Yusufu Salumu amewataka waandishi wa habari kuelimisha madereva juu ya umuhimu wa leseni na kuwataka madereva kuwa makini wanapoendesha vyombo vya usafiri  ili kuepuka
ajali za kizembe.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top