Latest News

Athari ya mvua katika jiji la Dar es Salaam; hapa ni kituo cha kupakia na kushusha abiria eneo la Karume,Ilala jijini humo. Kama picha inavyoonekana, kibanda cha kusimama abiria na kujikinga na jua au mvua kikiwa kimeezuliwa huku maji yakiwa yametapakaa kila sehemu kituoni hapo.
Askari  wa jiji wakishughulika katika kulifunga tairi la gari lililoegeshwa kinyume cha sheria katikati ya jiji ambapo mmiliki wake atatakiwa kulipa kiasi cha shilingi elfu 50 kama faini ya kosa hilo.
Askari wa jiji akiongea na mmoja aliyekutwa ndani ya gari alipoulizwa anajua kuendesha akajibu hapana lakini dereva kaingia ofisini mara moja ndipo mgambo akachukua hatua ya kulifunga kabisa.
Gari ndogo aina Starlet ikiwa imefungwa mara baada ya kupaki eneo ambalo haliruhusiwi kufanya hivyo

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top