Latest News

Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuri

SERIKALI ya Tanzania, imetoa kwa makusudi, kandarasi ya mabilioni ya fedha kwa wakandarasi na wataalamu wengine wazalendo kwa nia ya kuunga mkono wanataaluma Watanzania na kuwapa nafasi kubwa zaidi katikakuchangia maendeleo ya nchi yao.
 

Kandarasi hiyo ni ujenzi wa Daraja la Mto Mbutu, Wilayani Igunga, daraja ambalo ujenzi wake utawanufaisha maelfu ya wananchi katika wilaya hiyo na wilaya za jirani za Iramba Mkoani  Singida, Meatu Mkoani  Simiyu na Kishapu Mkoani Shinyanga.
 

Kandarasi hiyo ina thamani ya Sh. Bilioni 11. 3 huku  kazi ya usimamizi, ushauri na ujenzi wa daraja hilo kwa asilimia 100 utakuwa moja kwa moja kwa mikononi mwa wataalamu kutoka Tanzania
 

Kandarasi hiyo ilitangazwa wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipoweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Daraja hilo ambalo wataalam hao wazalendo wameahidi kuwa ujenzi wake utakamilika ifikapo Novemba, mwaka huu.
 

Miongoni mwa wataalamu hao wazalendo waliopewa kandarasi hiyo ni pamoja na makampuni 13 ya makandarasi, makampuni ya washauri na makampuni ya wasimamizi. Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli alimwambia Rais Kikwete kuwa kandarasi hiyo imetolewa kwa wataalam wazalendo kulingana na ahadi ambayo Rais aliitoa wakati alipozungumza na wataalamu hao wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya kuundwa kwa vyama vya kitaalamu vya sekta ya ujenzi mwaka juzi 2011. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top