MOURINHO ‘SPECIAL ONE’ KUZURU OLD TRAFFORD.

Pia amkaribisha Ferguson, Santiago Bernabeu
Kocha wa timu ya Real Madrid Jose Mourinho
Kocha wa Real Madrid  Jose Mourinho atahudhuria mechi baina ya klabu hasimu nchini Uingereza ambapo atashuhudia wapinzani wake katika ligi ya mabingwa Ulaya Manchester United watakapoikaribisha Liverpool katika dimba la Old Trafford.

Kocha huyo amesema anapenda kuwaona wapinzani wake wakicheza LIVE badala ya kuwafuatilia kupitia katika vituo vya Luninga.

Anasema mechi kati ya Liverpool na Manchester United itakuwa mechi kali ya kusisimua huku akijinasibu kwamba ataingalia mechi hiyo kama sehemu ya burudani na kazi yake.

Real Madrid itacheza na Manchester United katika ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora Februari 13 katika dimba la Santiago Bernabeu huku mechi ya marejeano ikipigwa Machi 5.

WACHEZAJI 41 WAFUNGIWA MAISHA KOREA KUSINI

Wachezaji 41 wamefungiwa kutocheza soka baada ya kupatikana na hatia ya upangaji wa matokeo katika ligi kuu nchini Korea Kusini.

Shirikisho la Kandanda ulimwenguni FIFA limethibitisha adhabu hiyo huku likidokeza kwamba uchunguzi ulifanywa kuanzia mwaka 2011.

Serikali nchini humo imeunga mkono adhabu hiyo kutokana na kukithiri kwa upangaji wa matokeo katika ligi ya nchi hiyo maarufu kama K-League pia katika Volleyball,Baseball na michezo mingine.

MESSI AMPIGIA SALUTI GERD MUELLER
Lionel Messi mchezaji bora
Lionel Messi Akishikilia Tuzo yake
 Licha kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara ya nne,Lionel Messi amemvulia kofia gwiji wa zamani wa Ujerumani na Bayern Munich kuwa alikuwa chuma cha pua enzi za uchezaji wake.
Lionel Messi alisema anamheshimu Mueller kwa soka lake la uhakika na historia itendelea kumkumbuka hivyo.
Messi (25) raia wa Argentina alivunja rekodi ya Mueller ya kufunga magoli 85 mwaka 1972 lakini yeye amefunga magoli SITA zaidi mwaka 2012 pekee kwa kufunga magoli 91.

PSG YAMKANA CRISTIANO RONALDO
Christiano Ronaldo
Mkurugenzi wa mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu nchini Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain Leonardo amekanusha uvumi ulioenea kuwa mshambuliaji wa klabu ya Real  Madrid  CRISTIANO DOS SANTOS RONALDO yuko mbioni kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini ufaransa.
Hata kocha Carlo Ancelotti wa PSG amekanusha uvumi huo.
Ikumbukwe kuwa mshambuliaji huyo kutoka nchini ureno mwanzoni mwa msimu huu alisema kuwa anafuraha kuendelea kuichezea klabu ya Real  Madrid baada ya kuongezwa kwa ushuru nchini uhispania.

Lakini naye kiungo wa klabu ya Swansea Pablo Hernandez amesema anaamini kuwa mashabiki wa klabu ya Chelsea the blues watampa mda wa kutosha kocha wa klabu hiyo Mhispania RAPHAEL BENITEZ ili klabu hiyo iweze kutulia.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top