Askofu
Desiderius Rwoma
Askofu D. Rwoma and Askofu Nestor Timanywa wakiwa katika basi na Maaskofu wengine
Askofu Rwoma (Wa kwanza) akiwa na Maaskofu wengine wa Bukoba
Askofu Rwoma na Askofu Dallu wa Geita
Askosu Rwoma na Askofu Kilaini wakiwa Singida
Askofu Rwoma akiwa na wanaseminari Singida
Askofu Rwoma baada ya kutoa upadirisho Mkoani Singida
Waamini
na wapenzi wa Bukoba na Kagera wamefurahi sana kumpata Baba Askofu
Desiderius Rwoma kama askofu wa Jimbo la Bukoba kumrithi askofu Nestor
Timanywa ambaye amestaafu kufuatana na sheria za kanisa.
Askofu
Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika parokia ya Rutabo,
Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean
Kardinali Rugambwa.
Alipata upadrisho kwa mikono ya Baba Askofu Nestor Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo.
· Akiwa
jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya
Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya
kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara
kati ya shule 10 bora kitaifa.
Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo
anawajua vizuri na wanampenda.
· Vile
vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia
wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila
mara amekuwa karibu nao.
· Kabla
ya kuteuliwa kuwa askofu wa Singida alikuwa makamu wa askofu wa Bukoba
na hivyo kulijua jimbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii
vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida.
· Akiwa
askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi.
Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo.
Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo
kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo
vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk.
· Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa Walei
Askofu
Desiderius Rwoma ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda
maendeleo. Ana uhusinao mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia,
kabila, taifa au dini.
WANABUKOBA NA WANAKAGERA WANAKUKARIBISHA KWA FURAHA NA SHANGWE, KARIBU NYUMBANI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment