Mamlaka ya
hali ya hewa (TMA) imetoa tahadhari kwa wananchi kuwa kutakuwa na mvua kubwa kuanzia
Januari 30, 2013 hadi Februari mosi 2013. Mvua hizi, zinatarajiwa kunyesha kwa kiwango
cha zaidi ya milimita 50 kwa muda wa masaa 24 kila siku.
Maeneo
yanayotarajiwa kuathirika zaidi ni mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani,
Mtwara na maeneo jirani na mikoa hiyo.
Imeelezwa kuwa chanzo cha mvua hizi ni
kuwepo kwa kimbunga cha “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo yaliyotajwa hapo juu.
Mamlaka imeendelea kueleza kuwa wakazi
wa maeneo hatarishi, watumiaji wa bahari na nchi kavu wanashauriwa kuchukua
tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na maafa zinashauriwa kuchukua hatua zinazofaa
kukabiliana na mvua hizi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment