WADAU WAONGEZEKA UCHAGUZI WA TFF
Idadi ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania
uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo
wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia
26.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu
hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10
kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua leo ni Michael Wambura anayewania umakamu
wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin
Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.
Idadi kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan
Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao
kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel
Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu),
Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph
Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani
Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na
Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid
Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani
Damoder (Dar es Salaam).
Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu
mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
UCHAGUZI TAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa
Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi
wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki,
mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha
muhtasari wa mkutano uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA
kabla ya keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
Mkoa utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda
uliotolewa utakosa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea
watano. Wagombea hao ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu
Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao
wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Yanga Kujipima kwa
Black Leopards
Mabingwa
Afrika Mashariki na kati ,Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam ,wanataraji kushuka
ugani katika katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya
Afrika Kusini. Kocha mkuu wa timu hiyo Ernie Brandts amesema kuwa kikosi chake
kipo fiti kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara.
Kocha huyo amesema kuwa anaamini vijana wake wamejinoa vilivyo walipokuwa Uturuki huku akitaraji kufanya vizuri katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Black Leopards.
Black Leopards inashiriki ligi kuu Afrika Kusini ikiwa
nafasi ya 12 katika ligi kuu nchini humo maarufu kama PSL ambayo inashirikisha
timu 16.Timu hiyo inataraji kuwasili hapa nchini Alhamisi wiki hii.
Akizungumzia mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara,kocha
Brandts amessema kuwa anataraji kupata upinzani wa hali ya juu kutokana na timu
TANO za juu kujiimarisha zaidi kwa maandalizi kamambe. Licha ya kutoshinda
mechi katika ziara ya timu yake nchini Uturuki kocha Brandts amesema kuwa
vijana wake watakuwa wamepata uzoefu wa mechi za kimataifa ambapo walicheza
mechi tatu na y a wikiendi hii dhidi ya Black Leopards itakuwa mechi ya NNE.
Kwa mujibu wa waratibu wa mechi ya Yanga na Black Leopards
kampuni ya Prime Time Promotion wametangaza kiingilio kuwa kati ya
shilingi ELFU TANO na ELFU THELATHINI. Katika hatua nyingine klabu hiyo
inataraji kufanya mkutano mkuu Jumapili wiki hii ambao utafanyika katika ukumbi
wa Police Officers Mess jijini Dar es Salaam.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment