Add caption
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mazishi ya mpigania uhuru na mwana ukombozi wa Afrika Komredi Landa John Nkomo yaliyofanyika jijini Harare katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare

Komredi Nkomo hadi anafikia mauti alikuwa Makamu wa Rais was Zimbabwe na Makamu Mwenyekiti wa Chama kilichopigania uhuru wa nchi hiyo cha ZANU-PF Kilicho chini ya Rais Robert Mugabe.


Katika mazishi ya shujaa Nkomo yaliyoongozwa na Rais Mugabe pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Zambia, Botswana na Namibia.

Akilihutubia taifa Rais Mugabe alisema, Hayati Nkomo alikuwa mfano thabiti wa amani katika Afrika na hata wakati anapelekwa Afrika Kusini kutibiwa kabla ya mauti kumfika, alikuwa kinara katika mazungumzo ya
kufikia mkataba wa Makubaliano ya vyama vya siasa juu ya Katiba itakayotumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao nchini Zimbabwe,


Licha ya kuhudhuria mazishi ya Hayati Nkomo, Dk.Bilal pia alipata fursa ya kumtembelea Rais Mugabe ofisini kwake Ikulu jijini Harare na kisha kukutana na baadhi ya Watanzania waishio Zimbabwe.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top