Mh. John P. Magufuri
Watendaji wa bodi ya mfuko wa barabara wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ili  kuongeza tija kwa taifa.

Akizindua bodi ya awamu ya tatu ya  mfuko na wakala wa barabara na Waziri wa Ujenzi Dakta John Magufuli  amesema watendaji waliomaliza muda wao wamefanya kazi nzuri kwa kujenga barabara.

Aidha Dakta Magufuli amewataka watendaji wapya wa bodi hizo kufanya kazi nzuri zaidi kuliko waliyofanya waliopita kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

Naye mwenyekiti mpya wa bodi mfuko wa barabara James Wanyancha amesema wamejipanga kubuni vyanzo vipya vya mapato  kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo mamlaka ya mapato Tanzania TRA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top