Deus Kibamba |
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha taifa kwa
wananchi TCIB Deus Kibamba alipokuwa akifafanua kuhusu chaguzi za madiwani
katika kata 29 Tanzania bara zilizofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Mkurugenzi huyo amesema amesema vyama vimekuwa vikiangalia
masuala ya kitaifa kwa kuelemea itikadi za vyama badala ya kuzingatia maslahi
ya taifa hivyo kudhoofisha maendeleo.
Bwana Kibamba amesema kuwa kuna upungufu mkubwa katika
kuhakikisha demokrasia inastawi hapa nchini kutokana na ushiriki duni wa
wananchi katika chaguzi ambao umetajwa kuhatarisha maendeleo ya demokrasia.
Katika hatua nyingine viongozi wa umoja huo wameoneshwa
kushangazwa kwa baadhi ya madiwani kuombeana mabaya kiasi cha kufikia hatua
kushikana uchawi,huku wengine wakishindwa kufanya kazi kwa kuugua tangu
kuchaguliwa kwao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment