IGP Said Mwema |
Tukio hilo lilitokea
Desemba 15 katika kijiji cha Mgoma Tarafa ya Kanazi, Wilaya ya Ngara na kusababisha vifo vya askari wawili na timu
hiyo inayohusisha Idara ya Upelelezi na Kamisheni ya Oparesheni ili
kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Timu hiyo itaungana na
timu ya upelelezi ya Mkoa kuchunguza zaidi tukio hilo na kuwabaini wote
waliohusika katika kusababisha vifo kwa askari na raia pamoja na madhara
mengine dhidi ya mali.
Wakati uchunguzi huo ukiendelea, Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa watulivu, hususani wananchi wa Mkoa wa Kagera na waendelee kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jeshi la Polisi ili wahalifu hao wachache wanaotumia kisingizio cha hasira kali waweze kukamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment