Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limesema
kuwa hali duni na mazingira magumu ya wafanyakazi yanasababisha kushuka kwa
ufanisi mahala pa kazi hivyo kupunguza tija kwa taifa.
Katibu mkuu wa TUCTA Nicolas
Mugaya amesema kuwa wafanyakazi wengi wanalipwa mishahara duni huku wakikatwa
kiwango kikubwa cha kodi pia wakijitahidi kupambana na mfumuko wa bei unaopanda
kila uchao.
Bwana Mugaya amesema katika sekta binafsi imefikia mtu kulipwa
kima cha chini shilingi elfu 70 huku waajiri wakitoa kisingizio kwamba serikali
haijaweka kianzio cha kiasi cha mshahara wa kima hicho.
Kuhusu sheria ya mifuko ya jamii ,katibu huyo wa TUCTA amesema
kuwa kuna umuhimu wa kuwepo kwa kipengele cha kujitoa katika mifuko hiyo
kutokana na kwamba kuna aina ya kazi ambazo wafanyakazi hawawezi kufanya kazi
na kufikisha umri wa kustaafu wa miaka 55 – 60.
Imeelezwa kuwa mazingira ya kazi kama vile migodini na ajira
za mikataba ambayo mara nyingi mfanyakazi anaweza kuacha kazi kwa sababu za
kiafya lakini kwa mujibu wa sheria atalazimika kusubiri fedha zake mpaka umri
uliowekwa kisheria .
Katibu huyo amesema kuna madai mengi lakini hawajafanikiwa kuonana
na Rais kama walivyoahidiwa mwaka huu hivyo wanaangalia kipindi kingine ambacho
wanaweza kukutana kwa ajili ya kujadili madai yao kwa serikali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment