Mkazi wa Mwasanga jijini
Mbeya Sosteli Mponzi (kulia) akimuonyesha Victoria Zitta Mnyanyi
(kushoto) ambaye ni Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe tawi
la Mbeya moja ya nyumba ya kale iliyokuwa inatumiwa na kabila la wasafwa
ambalo ni kabila maarufu mkoani humo. Mponzi ameamua kujitolea kujenga
kituo cha utamaduni wa kabila hilo ambacho kitatunza kumbukumbu za
utamaduni na mila zote ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo
yaliyofanywa na mababu zao.
Msafwa wa Mwasanga
jijini Mbeya Ibrahim Saimon akipuliza pembe ya Mnyama aina ya Tandala
“Ndundwe” iliyokuwa inapingwa wakati wa sherehe za kumaliza msiba
“matanga” za kabila la wasafwa. Sosteli Mponzi ameamua kujitolea kujenga
kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila hilo ili kizazi kijacho
kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi ya wasafwa wa
Mwasanga jijini Mbeya wakimuangalia Mary John akisaga unga wa ulezi kwa
kutumia jiwe aina ya “Lwala” wakati walipotembelea ili kujionea ujenzi
wa kituo cha utamaduni wa kabila lao kinachojengwa kwa kujitolea na
Sosteli Mponzi. Baadhi ya wasafwa waishio maeneo ya vijijini bado
wanasaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe hilo kwa ajili ya kutengenezea
pombe.
Mkazi wa Mwasanga jijini
Mbeya Sosteli Mponzi (kushoto) akimuonyesha Victoria Zitta Mnyanyi
ambaye ni mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya
mti wa asili aina ya msulusulu ambao wazee wa kabila la wasafwa walikuwa
wakiutumia kwa ajili ya kutibu mifugo. Mponzi ameamua kujitolea kujenga
kituo cha utamaduni wa kabila hilo ili kumbukumbu zisiweze kupotea
kwani hivi sasa kutokana na utandawazi makabila mengi yamekuwa
yakipoteza utamaduni wao.
Baadhi ya wasafwa wa
Mwasanga jijini Mbeya wakicheza ngoma aina ya Mbeta ya kabila hilo
ambayo inachezwa wakati wa kumaliza msiba “Mwengulo” kama walivyokutwa
na mpiga picha wetu hivi karibuni alipotembelea kituo cha kutunza
utamaduni na mila za kabila la wasafwa. Ujenzi wa kituo hicho unajengwa
kwa kujitolea na Sosteli Mponzi ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo
yaliyofanywa na mababu zao.
Mkazi wa Mwasanga jijini
Mbeya Juma Changa akionyesha jinsi wazee wa zamani walivyokuwa
wakichonga mpini wa jembe kwa kutuma teso “menzo” wakati mpiga picha
wetu alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila la
wasafwa huku Said Mbata (kulia), Victoria Zitta Mnyanyi (katikatia) na
Sosteli Mponzi (kushoto) wakimuangalia. Ujenzi wa kituo hicho unajengwa
kwa kujitolea na Mponzi ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo
yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi ya wasafwa wa
Mwasanga jijini Mbeya wakimwonyesha mpiga picha wetu jinsi wazee wa
zamani wa kabila hilo walivyokuwa wanakunywa pombe aina ya Kimpumu
wakati alipotembelea kujionea ujenzi wa kituo cha kutunza utamaduni na
mila za kabila hilo.Kutokana na kuenea kwa magonjwa mbalimbali ya
kuambukiza hivi sasa kila mtu anakunywa pombe hiyo kwa kutumia chombo
chake.Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Kwa hisani ya http://ngwesa.blogspot.com
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment