Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura waraka wa
marekebisho ya Katiba, kwani wametimiza wajibu wao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema
marekebisho ya Katiba ni jambo muhimu, lakini lazima yapate ridhaa ya
wanaohusika ambao ni wajumbe.
“Nawasukuru
wajumbe kwa kupitisha jambo hili. Nawashukuru wote, waliokubali na
waliokataa. Ndivyo demokrasia ilivyo. Tulitaka waseme ndiyo au hapana,
hivyo tulitarajia kupata majibu yoyote kati ya hayo mawili.
Marekebisho
mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba
yetu inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya
utawala bora tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,”
amesema.
Jumla
ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70
waliunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya
kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura
zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.
Vipengele
vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama
ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya
Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile
Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho
ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo
ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua
wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano
Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika
Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe
wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
RAMBIRAMBI MSIBA WA AMINA SINGO
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya
kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa habari za michezo katika kituo cha
redio cha 100.5 Times FM, Amina Singo kilichotokea usiku wa kuamkia
jana.
Msiba
huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa
nyakati tofauti kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya
kazi na TFF, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka
daima.
Tutamkumbuka kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. TFF
tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na
marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina
SITA ZATINGA ROBO FAINALI UHAI CUP
Timu
sita zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya
Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20
(U20) wa klabu za Ligi Kuu ya Tanzania.
Hatua
ya robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Karume na
Chamazi, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa
kupitai maji Uhai itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo
hivyo.
Timu zilizofuzu kutoka kundi A
ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar
es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha na Ruvu Shooting ya Pwani
wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam pekee.
Katika
mechi zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu) Coastal Union na
Mtibwa Sugar zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
wakati Uwanja wa Azam ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting
mabao 2-1.
Nafasi
mbili za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B zinawaniwa na timu za
Simba, African Lyon na Polisi Morogoro. Mechi itakayochezwa leo saa 10
jioni katika Uwanja wa Chamazi kati ya Polisi Morogoro na Simba ndiyo
itakayoamua timu zitakazoungana na Azam kutoka kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment