Alikuwa akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Ugalla kata ya Ugalla mara baada ya kukagua mradi huo akiwa katika siku ya nne ya
ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Alisema
anawashukuru wakazi hao kwa kuibua mradi huo ili waweze kunufaika na maji ya
mto Ugalla ambao unapita jirani. Pia aliwataka waheshimu uamuzi wao wa kutoa
eneo hilo kwa mradi ili kuepuka migogoro ya umilikaji wa kifamilia na kiukoo.
“Ninawasihi
muelewane ili kuepuka migogoro ya maeneo. Mkishaanza kuvuna wako watakaodai
kuwa hapa nilipewa na babu yangu, hapa nilipewa na babu wa babu, wataanza kudai
fidia. Ni vema mkaelewana mapena juu ya umiliki wa eneo la
mradi,” alisema.
Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu ambaye
ni mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Umwagiliaji
Kanda ya Mbeya, Bw. Elibariki Mwendo alisema wamejenga tanki la kuhifadhi maji
lenye ujazo wa lita 530,000 ambazo zinaweza kumwagilia hekta 225.
Alisema
mitambo ya kupandisha maji kwenye tanki hilo itaendeshwa kwa kutumia nguvu ya
umeme wa jua pamoja na umeme unaozalishwa kwa nguvu ya upepo.
Mradi huo ulioibuliwa
na wananchi mwaka 2007 kupitia zoezi la fursa na vikwazo vya maendeleo,
umegharimu sh. milioni 778. Unamilikiwa
na wanachama 146 na utahudumia watu 3,077.
Kesho (Jumanne,
Desemba 18, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata ya Sitalike ambako atahutubia
wananchi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment