STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 17.12.2012
OFISI ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imeeleza kuwa miongozo na maelekezo
inayoyapata kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein imekuwa ni chachu ya mafanikio
inayoyapata na kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika kufikia
malengo yaliowekwa.
Maelezo
hayo yametolewa leo na uongozi wa Wizara hiyo, wakati wa mkutano kati
ya uongozi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein, katika kuangalia utekelezaji wa Malengo Makuu ya
Wizara hiyo kwa kipindi cha Aprili- Juni 2011-2012 na Julai- Septemba
2012-2013.
Katika
mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Katibu Mkuu wa
Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee
na Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji Balozi Mohamed
Ramia Abdiwawa.
Akisoma
taarifa ya utangulizi ya utekelezaji wa Malengo makuu hayo ya Wizara,
Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame alitoa shukurani za
pekee kwa Dk. Shein kwa namna anavyotoa miongozo ya kiutendaji ambayo
imesaidia sana kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo.
Dk. Mwinyihaji, alieleza
malengo iliyojipanfia Ofisi hiyo ambapo miongoni wma malengo hayo ni
pamoja na kuendeleza Umoja wa Kitaifa na mashirikiano, kuendeleza
jitihada za kufanya mageuzi ya Serikali za Mitaa ikiwemo kufanya mapitio
ya mipaka ya maeneo pamoja na kusimamia utungaji wa Sheria na
kuimarisha na kuongeza uwezo wa Idara Maalum za SMZ.
Malengo
mengine ni pamoja na kuratibu na kusimamia ulinzi na usalama,
kuimarisha huduma bora katika vyuo vya mafunzo pamoja na kupunguza
msongamano, kuimarisha mfungamano wa kikanda ili Wazanzibari waweze
kutumia fursa za kiuchumi zinazotokana na Jumuiya za Afrika Mashariki,
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Jumuiya nyengine za
Kikanda.
Aidha,
Dk. Mwinyihaji alitaja malengo mengineyo ambayo ni kutoa elimu ya
kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na VVU, kuratibu utekelezaji wam
kiradi ya wananchi, kuratibu shughuli zinazotekelezwa na sekta zikiwemo
elimu, afya, kilimo, maji na miundombinu pamoja na kuwashajiisha
Wazanzibari wanaoishi nchi za nje katika kushiriki na kuchangia
maendeleo ya kijamii na kiuchumi na mengineyo.
Ofisi
hiyo pia, ilieleza jinsi inavyoendelea na miradi yake ya maendeleo
ukiwemo mradi wa mawasiliano Ikulu, ujenzi na ukarabati wa majengo ya
Ikulu na nyumba za Serikali, mradi wa uendelezaji wa vitambulisho,
ujenzi wa Chuo kipya cha Mafunzo Hanyegwa Mchana, mradi wa shamba la
mbogamboga Bambi na miradi mengineyo.
Aidha,
Dk. Mwinyihaji alieleza kuwa Zanzibatr imepatiwa heshima kubwa kwa
kukubalika kuwa ni kitovu cha lugha ya Kiswahili katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Sambamba
na hayo, Zanzibar imepewa nafasi moja ya ajira katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambayo ni ya Usimamizi wa Masuala ya Madawa ambapo nafasi
hiyo ameipata Bi Hidaya Juma Hamad wa Zanzibar.
Pia,
Zanzibar imekuwabaliwa miradi yake katika EAC ambapo mradi wa Uingizaji
na Uhamishaji wa bidaa, mradi ambao utaiwezesha Zanzibar kufanya
upembuzi yakinifu katika bandari yake kuu. Ambapo mradi huo pia,
utazinufaisha bandari za Dar-es Salaam, Tanga na Mombasa na tayari jumla
ya Dola za Kimaerekani milioni 500 zimetengwa.
Dk.
Mwinyihaji alieleza kuwa hivi sasa Ofisi hiyo inaendelea na mazungumzo
kati yake na Kampuni mbili zenye azma ya kusimamia usafi wa miji ikiwemo Kampuni ya ZANREC Plastic Limited ambayo ina azma ya kuzoa taka zote za plastic.
Pia,
Kampuni ya SYNCHRONA Waste Management ya Marekani, inatarajia kuzalisha
umeme kutokana na taka utakaofikiwa MW 30, ambapo Kampuni hii piam
itakusanya kwa makubaliano maalum taka zote za Unguja na Pemba.
Hata
hivyo, Dk. Mwinyihaji alieleza kuwa mikakati ya kutatua changamoto za
kuwaondosha wanyama wanaozurura mjini, udhalilishaji wa watoto kijinsia
na ubakaji katika Wilaya na Mikoa imewekwa ikiwa ni pamoja na kuunda Kamati ya kusimamia na kuondosha wanyama wanaozurura.
Nae Dk. Shein kwa upande wake alitoa
pongezi kwa Wafanyakazi, viongozi na Watendaji wote wa Ofisi hiyo kwa
kuendelea kushirikiana pamoja katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni
pamoja na kuwasilisha utekelezaji wa malengo makuu ya Ofisi hiyo kwa
ufanisi mkubwa.
Dk.
Shein alisisitiza haja ya kuendeleza mashirikiano kwani ndiyo
yanayoleta maendeleo kwa nchi na wananchi wake huku akisifu mashirikiano
anayoyapata kwa upande wake katika kuwaletea maendeleo wananchi wote.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment