Wakati kesho ni sikukuu ya Krismasi, maelfu  ya waumini wa dini hiyo wako kwenye maandalizi ya mwisho ambapo wamelalamikia kupanda bei za bidhaa hasa mavazi na vyakula katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu hiyo

Hayo yamesemwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipoelezea wakati wa mahojiano maalum kuelezea maandalizi ya kuelekea sikuku za Krismas hapo kesho.
Ingawa uchumi unasemekana kukua kwa asilimia 6 kwa mwaka huu lakini bado garama za maisha zimeendelea kuwa changamoto kwa wananchi mbalimbali kwa kutoona angalau ya unafuu wa maisha.

ADOLF MKENDA ni mkuu wa idara ya uchumi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam amesema kupanda kwa gharama za maisha kunasababishwa na mahitaji makubwa ya bidhaa ambazo huwa adimu kwa kipindi cha sikukuuu.
Bwana Mkenda amesema sababu nyingine ya kupanda kwa gharama za maisha kunasababishwa na kwa gharama za  usafirishaji  na usambazaji wa chakula kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Mchumi huyo pia ameelezea tathmini ya mwaka huu na changamoto zake na kuwataka wananchi kujituma katika kufanya kazi ili kuwa na angalau ya maisha katika mwaka ujao.

Kesho ni siku kuu ya Krismass ambapo Wakristo ulimwenguni kote wanaungana katika kuadhimisha  kumbukumbu ya  kuzaliwa kwa mkombozi wa ulimwengu Yesu kristo takribani miaka 2000 iliyopita




TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top