Wito umetolewa kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Wabunge pamoja na Madiwani kuhakikisha wanasimamia majimbo yao ili kuleta maendeleo katika nchi.
Akizindua mradi wa mabasi yaendayo kasi Waziri wa TAMISEMI bi.Hawa Ghasia amesema  mradi unalenga  kutoa huduma bora na nafuu jijini Dar es salaam kwa  kuleta ukuaji wa uchumi endelevu kwa wananchi.
 Waziri huyo amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo Kutakuwa ni kichocheo cha kuimarika kwa sekta nyingine za umma na binafsi katika usafirishaji hivyo kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka.

Pia bi.Ghasia amesema  huduma zinazotolewa katika  usafirishaji  ziangalie pia watu weye kipato cha chini ili kuwawezesha kumudu gharama za usafiri kama ilivyo kwa watu wenye kada ya juu.
Naye Mstahiki Meya bwana Oscar Ngatare amesema kuwa Lengo la kuwakutanisha viongozi hao Wabunge pamoja na Madiwani ni kuhusiana na mikakati ya kuleta maendeleo katika jiji la Dar es salaam zoezi hilo lina tegemewa kuanza mwezi Julai mwaka ujao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top