Kamanda Kova |
Jeshi la polisi kanda maalum limesema kwamba liko imara
kukabiliana na vitendo vya uhalifu hasa katika kipindi cha msimu wa sikukuu za
Krismas na mwaka mpya.
Kamanda wa Polisi kanda maalum Dar es Salaam amewataka
wananchi kutumia muda huo kusherehekea kwa amani na utulivu huku waumini
kutumia muda vizuri kwa ajili ya ibada bila uvunjifu wa sheria za nchi.
Kamanda Kova amesema kuwa wakati wa sherehe za Krismas waumini
wa dini ya Kikristo wamekuwa wakiabudu makanisani lakini sherehe huwa na
muendelezo katika maeneo mengine ambayo mara nyingine vitendo vya uhalifu
hujitokeza.
Katika kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati
wa sikukuu jeshi hilo limewataka wamiliki wa kumbi za starehe kuhakikisha
wanaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria zilizowekwa huku jeshi hilo
likitoa tahadhari kwa wananchi watakaotembelea fukwe za bahari kuwa makini.
Pia Jeshi hilo limewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa
jeshi hilo pindi kunapokuwa na ishara ya
kutokea kwa uhalifu au vinapotokea vitendo hivyo na askari wako tayari
kuwashughulikia kisheria watakahusika na uvunjifu wa amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment