Nchini Uingereza imefahamika kwamba
vifaa vyote vya kisasa vinavyotumika majumbani vyenye uwezo wa
kuunganishwa kwenye mtandao wa internet vitawekewa vizuizi vya picha za
ngono ama pengine familia ziamue kupokea picha hizo zitaachwa zijimalize
zenyewe na watoto wao, hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Uingereza, David
Cameron.
Kwa kuongezea,waziri mkuu wa Uingereza ,kuzuia picha za
ngono mtandaoni na ubakaji vitakuwa ni kinyume cha sheria kwa England na
Wales na baadaye itafuatia Scotland.
Bwana Cameron ametoa onyo
hilo wakati alipokua anatoa hotuba yake kuhusiana na ngono mtandaoni na
kueleza kuwa kunadumaza watoto na utoto na akaeleza kuwa wateja wa sasa na
wapya watahusika na sheria hiyo mpya.
Onyo hilo la waziri mkuu wa
Uingereza linakuja miaka saba baadaye wakati ambapo David Cameroon
aliwahi kuwaambia Google kwenye mkutano kwamba wanasiasa wanapaswa
kushawishi makampuni kubadilisha na sio kubadili sheria hizo.
Na
leo ametangaza kwamba amefanikiwa kufikia makubaliano na makampuni
makubwa manne juu ya kuweka chujio la picha za ngono, baada ya matukio ya
nyuma ya pazia kuwa na sehemu kama hizo.
Pia akadokeza kuwa endapo
makampuni makubwa kama google hawatakubaliana na wito huo wa kuzuia
masharti ya utafutaji ,atatunga sheria.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment