Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza(Shati jeupe)
akiangalia zao la Mahindi yaliyolimwa katika Bustani Maalum ya Shamba
Darasa katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo
kujionea Kilimo cha Kisasa na Biashara Maonesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Mtaalam wa Kilimo wa
Jeshi la Magereza, Mrakibu wa Magereza, Uswege Mwakahesya.
Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza akiangalia zao
la Kitunguu kinachozalishwa na Jeshi la Magereza katika Gereza Mang’ola
Mkoani Arusha alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza, Maonesho ya 38
ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Waziri Chiza
ameahidi kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kutafuta fursa ya
Masoko ya ndani na nje ya nchi(wa pili kulia ni Afisa Masoko wa Shirika
la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda.
Muonekano
wa Bustani ya Shamba Darasa katika Banda la Jeshi la Magereza lililopo
katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ambapo sehemu kubwa ya
Wananchi wananufaika na Elimu ya Kilimo cha Kisasa na chenye tija katika
Maonesho hayo yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza(Shati jeupe)
akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari baada ya kutembelea Bustani
Maalum ya Shamba Darasa ya Jeshi la Magereza iliyopo katika Maonesho ya
38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Katika Mahojiano hayo
Mhe. Waziri ameahidi Kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kutoa
elimu ya Kilimo Bora kwa Wakulima hapa Nchini pamoja na kulisaidia Jeshi
hilo ili kupata fursa mbalimbali ya kupata Wawekezaji wa ndani na nje
ya nchi katika masuala ya Kilimo.
Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza akiondoka katika
Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo Julai 7, 2014
katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar
es Salaam.
0 comments:
Post a Comment