JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika baadhi ya magazeti ya leo tarehe 27 Juni, 2014 kuna Taarifa
zisizo sahihi likiwemo gazeti la Uhuru lenye kichwa cha habari “BILA
KUPITIA JKT HAKUNA AJIRA SERIKALINI na gazeti la Tanzania Daima lenye
kichwa cha habari “IKULU: RUSHWA YA NGONO IMEKITHIRI SERIKALINI”.
Magazeti yote haya yameandika habari za kupotosha Umma kuhusu hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue aliyoitoa tarehe 26/6/2014 katika mkutano wa Mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Makatibu Tawala uliofanyika mjini Dodoma. Magazeti hayo yamejenga taswira kwamba Katibu Mkuu Kiongozi alitoa taarifa kwamba “Hakuna ajira bila kupitia Jeshi la Kujenga Taifa” na “Rushwa ya ngono imekithiri Serikalini”.
Serikali inapenda kutoa ufafanuzi kwamba taarifa hizo siyo za kweli wala hazielezi taarifa halisi aliyoigusia Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Katika hotuba yake alisema “Aidha, ningependa mjue kuwa kuanzia sasa tutaweka mkazo mkubwa sana kwenye sifa ya uzalendo kwenye ajira Serikalini. Hatuwezi kuwa na Watumishi wa Umma ambao hawana uzalendo.Pale ambapo waombaji kazi kwenye Utumishi wa Umma wana sifa zote sawa, lakini wakawepo wale ambao wamepitia Jeshi la Kujenga Taifa watapewa kipaumbele.lakini narudia, kipaumbele hicho kitumike pale tu ambapo sifa zingine zote ziko sawa, na si vinginevyo”.

Kuhusu suala la rushwa ya ngono lililoripotiwa na gazeti la Tanzania Daima, si kweli kwamba Katibu Mkuu Kiongozi alisema kumekuwa na ongezeko aukukithiri kwa rushwa ya ngono katika utoaji wa ajiraserikalini. Alichokisema Katibu mkuu kiongozi ni kwamba “Lakini bado malalamiko yanasikika kuwa ati huwezi kuajiriwa kwenye Utumishi wa Umma isipokuwa kama unajulikana au unatoa rushwa, ama ya fedha au ya ngono. Jambo hilo linanisononesha sana. Mimi naamini mambo hayo yamepungua sana. Lakini kama yanafanyika, ni kinyume kabisa na Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na lazima tulio katika ukumbi huu tuyapige vita kwa bidii zote, bila kuoneana haya, hadi wananchi waone kuwa kweli hayapo. Tusipuunze hata kidogo malalamiko ya wananchi, bali tujichunguze na tuchunguzane, ili kama mambo hayo bado yapo, kwa pamoja tuazimie kuyakomesha kabisa kwenye Utumishi wa Umma”. Hotuba halisi ya Katibu Mkuu Kiongozi inaweza kupatikana kwenye website ifuatayo www.chiefsecretary.go.tz
27/6/2014
0 comments:
Post a Comment