Shughuli zinafanywa leo kukumbuka tukio la karne
kamili iliyopita mjini Sarajevo, ambapo mrithi wa mfalme wa mamlaka ya
Austria-Hungary aliuliwa na mzalendo wa Serbia na kuwa chanzo cha kuzuka
Vita vya Kwanza vya Dunia.
Vilembwe vya prince huyo, Franz Ferdinand, watahudhuria gwaride litalofanywa katika kasri yao karibu na Vienna, Austria.
Princess Anita Hohenberg, kilembwe cha Franz Ferdinand, aliiambia BBC kwamba Franz Ferdinand daima hakupenda vita:
"Baba wa babu yangu angeshtushwa, angeshtuka kabisa, kwa sababu akijua upungufu wa jeshi lake, kwa sababu alikuwa mkuu wa jeshi.
Vita hivyo vilikuwa vibaya, vibaya sana."
Austria sasa haina mfalme.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment