TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAUTANGAZIA UMMA KUEPUKANA NA
MATAPELI WANAOCHUKUA FEDHA KWA LENGO LA KUWAPATIA VIJANA NAFASI ZA
KUJIUNGA NA JKT. NAFASI ZA KUJIUNGA NA JKT HAZIUZWI POPOTE.
JESHI LINAOMBA UMMA UTAMBUE KUWA LINAENDESHA MAFUNZO YA AINA
MBILI. AINA YA KWANZA NI YA KUJITOLEA NA AINA YA PILI NI YA MUJIBU WA
SHERIA.
NAFASI ZA VIJANA WA KUJITOLEA ZINATOLEWA NA MKUU WA JKT
KUPITIA WAKUU WA MIKOA TANZANIA BARA NA VISIWANI. AIDHA WAKUU WA MIKOA
HUZIGAWA NAFASI KWA WAKUU WA WILAYA, NAO WAKUU WA WILAYA HUGAWA KATIKA
TARAFA, KATA NA VIJIJI VYAO.
AINA YA PILI NI YA MUJIBU WA SHERIA KWA VIJANA WANAOHITIMU
KIDATO CHA SITA KATIKA MWAKA HUSIKA NA MAJINA YAO YANATOLEWA NA WIZARA
YA ELIMU NA UTAMADUNI KUPITIA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA.
JAMII INATAHADHARISHWA KUACHA KUTOA FEDHA KWA MATAPELI KWA
NIA YA KUPATA NAFASI ZA KUJIUNGA NA JKT. KUTOA AU KUPOKEA RUSHWA NI
KINYUME CHA SHERIA. HIVYO MTOAJI NA MPOKEAJI WAKIGUNDULIKA
WATASHUGHULIKIWA KISHERIA.
0 comments:
Post a Comment