Serikali ya Iraq inasema kuwa
vikosi vyake vimeuteka mji wa kaskazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji
wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka wiki mbili zilizopita.
Vyombo vya habari vya kitaifa vimesema kuwa
wanajeshi wakisaidiwa na mizinga pamoja na ndege za kijeshi
waliwafurusha wanamgambo wa kundi la ISIS na kuwaua zaidi ya sitini.
Waasi hao wamesema kuwa kulikuwa na mapigano makali katika mji huo na kwamba mashambulizi hayo hayakufua dafu.
Iwapo itathibitishwa ,utekaji wa mji wa Tikrit
utakuwa hatua kubwa ya jeshi la Iraq tangu ISIS kuyateka maeneo mengi ya
Iraq kaskazini mapema mwezi huu.
Serikali sasa inasema kuwa inajiandaa kuelekea mjini Mosul ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.
Wakati huohuo Iraq inasema kuwa imepokea kundi
la kwanza la ndege za kijeshi ilizoagiza kutoka Urusi ili kuisadia
kukabiliana na wapiganaji wa dhehenu la kisunni ISIS ambao wameyateka
maeneo mengi ya taifa hilo.
Wizara ya Ulinzi inasema kuwa ndege hizo 5 zenye
uwezo wa kushambulia maeneo ya ardhini zitaaanza kuhudumu katika
kipindi cha siku chache zijazo,huku nyingine zikitarajiwa kuwasili.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment