Jeshi la Iraq linasema kuwa linafanya opersheni kubwa ya kuukomboa mji wa kaskazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa Kisunni.
Taarifa zinaeleza kuwa maelfu ya wanajeshi
wanakaribia mji wa Tikrit, ambao ulitekwa na wapiganaji wa ISIS zaidi ya
wiki mbili zilizopita pamoja na eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq.
Wapiganaji wa Kisunni wanasema raia wameuwawa na kujeruhiwa katika mapigano.
Katika siku mbili zilizopita eneo la chuo kikuu
cha mji wa Tikrit limeshambuliwa na wanajeshi wa serikali waliopelekwa
huko kwa helikopta.
Na Askofu wa Ibril, kaskazini mwa Iraq katika
eneo la kabila la Kurd, anasema maelfu ya Wakristo wamekimbia vijiji
karibu na Mosul katika siku za karibuni.
Askofu aliiambia BBC kwamba wapiganaji wa ISIS
wameshambulia maeneo mawili ya wakaazi wengi Wakristo, na eneo mojawapo
linalindwa na wapiganaji wa Kikurd.
Wakimbizi hao wamepata hifadhi katika jimbo la Wakurd la Iraq.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment