http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/06/rage.jpg

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage
 
SIMBA SC inatarajia kufanya mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu Kesho Jumapili (Juni 29 mwaka huu), katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kuelekea katika mkutano huo ambapo Simba inatarajiwa kumpata Rais mpya, makamu wa Rais na wajumbe wapya wa kamati ya utendaji kwa mujibu wa katiba mpya Simba, mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage awewatakia kila la heri wanachama wote katika uchaguzi huo.

 Rage amesema ana imani uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu ili klabu ipige hatua.

“Nawaomba wanachama wote hai wajitokeze ili watimize haki yao ya kidemokrasia”. Alisema Rage.

“Nawatakia uchaguzi mwema, nikiwa kama mwenyekiti sitakiwa kuwa upande wowote, kwahiyo nawatakia mkutano mwema wa uchaguzi”.

“Mimi kazi yangu itakuwa ndogo sana , kufungua mkutano na kuukabidhi mkutano kwa kamati ya uchaguzi”. Aliongeza Rage.

Shughuli za uhakiki wa wanachama zitaanza saa moja kamili asubuhi na Mkutano umepangwa kuanza saa tatu kamili asubuhi na wanachama na wagombea wote wanaombwa kuwa wamekaa katika viti vyao kufikia muda huo.

Katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea 27 wanatarajiwa kushiriki na Kamati ya Uchaguzi imeazimia kwamba suala la muda litazingatiwa sana safari hii kutokana na ukweli wa kuwepo kwa wagombea wengi.

Pia Kwenye uchaguzi huo kutakuwa na huduma ya kutoa kadi kwa washabiki wa Simba wanaotaka kuingia katika mfumo mpya wa Benki ya Posta.

Katika hatua nyingine, Rage aliwaasa wanachama na mashabiki hao kuichangia klabu hiyo kwa njia mfumo mpya walioanzisha na benki ya Posta Tanzania.

“Kwasasa hivi tumeshirikiana na klabu ya Dar Young Africans kuingia mkataba na benki ya Posta, nawaomba mashabiki wa Simba waliopo Tanzania nzima wapate kadi zinazoitwa `Simba Fan Card` ili waweze kuchangia kila mwezi shilingi elfu moja”.

“Tunategemea tukipata hela ya mashabiki angalau shilingi elfu 50 kwa mwezi, klabu yangu itakuwa na uwezo wa kupata si chini ya milioni miatano kwa mwaka”.

“ Pesa hii itaisaidia klabu kuendeleza uwanja na kufanya shughuli nyingine za klabu na kuifanya ijitegemee na sio kutegemea pesa za watu wachache”.

Hata hivyo amewaomba mashabiki na wanachama kufika maeneo ya Bunju kuona maendeleo ya ujenzi ya uwanja wa mazoezi.
“Unajua tangu klabu hii kuanza haijawahi kuwa na kiwanja cha mazoezi, tunaazima azima tu na nashauri viongozi watakaoingia madarakani wajue nimeacha uwanja na wao wajenge hosteli, mahali pa kuweka wachezaji ili kupunguza gharama.”.

“Unajua kwa mwaka tunatumia zaidi ya milioni 350 ambayo wanaweza kujenga Hosteli nzuri kwa kiasi hicho”.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top