Marehemu Abubakari Shariff Makaburi
Mhubiri mwenye utata aliyeuawa na polisi mjini
Mombasa Jumanne usiku, Abubakar Shariff Makaburi alizikwa usiku wa
manane kuamkia leo.
Maziko yake yalifanyika saa sita baada ya watu wasiojulikana kumuua akiwa nje ya mahakama ya Shanzu mjini Mombasa.
Aliwahi kuhojiwa na BBC na kukiri kuwa yuko
tayari kufa kama shahidi wa dini. Makaburi alisema kuwa alijua wazi
atauawa hasa baada ya mhubiri mwingine Sheikh Aboud Rogo ambaye alikuwa
anaeneza itikadi kali za kiisilamu mjini Mombasa kuuawa.
Makaburi aliuawa akiwa na mhubiri mwingine nje
ya mahakama punde tu baada ya kuhudhuria kesi ya washukiwa 29 wa ugaidi
mjini Mombasa.
Vijana hao walikuwa miongoni mwa wale
waliokamatwa nje ya msikiti Musa kutokana na harakati za polisi
kupambana na vijana wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu mjini humo
mwezi mmoja uliopita.
Duru zinasema kuwa Makaburi alizikwa usiku ili
kuzuia vurugu asubuhi yake kutoka kwa vijana waisilamu waliokuwa wameaza
kusababisha hali ya taharuki usiku mara baada Makaburi kuuawa.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment