Inaarifiwa kuwa watu kadhaa wamekufa na wengi kujeruhiwa katika msongamano kwenye uwanja wa michezo wa taifa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitali lakini maafisa hawana hakika watu wangapi wamekufa.

Mwandishi wa habari mmoja wa Ufaransa anasema aliona maiti saba.
Hayo yalitokea wakati wa kuajiri watu katika idara ya uhamiaji ya Nigeria.

Maelfu ya watu walijitokeza kufanya mtihani wa ajira - inaarifiwa mkanyagano ulitokea walipojaribu kufika katikati ya uwanja.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top