Juhudi za kimataifa zinaendelea kutafuta ndege ya
shirika la ndege la Malaysia iyokuwa ikielekea Beijing nchini China na
kupotea baharini ikiwa na abiria 239.
Ndege hiyo iliyopotea aina Boeing 777 ilkuwa na abiria wapatao 239 pamoja na wafanyakazi wa ndege.
Asia ya Kusini Mashariki imeongeza
nguvu katika juhudi hizo za kutafuta ndege hiyo iliyopotelea katika eno
la bahari la Malaysia na Vietnam .
Shirika la ndege la Malaysia limesema ndege hiyo
namba MN370 ilipotea majira ya saa 8:40 kwa saa Malaysia siku ya Ijumaa
baada ya kuondoa Kuala Lumpur.
Jeshi la Malaysia limesema kikosi cha pili cha
helikopta na Meli kimetumwa kwenye eneo la tukio lakini hata hivyo
hakuna chochote kilichoonekana katika hatua za awali za utafutaji wa
ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili Beijing China majira ya saa 12:30 kwa saa za Malaysia.
Waziri wa Usafiri wa Malaysia amesema hakuna taarifa za zozote za kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo.
"Tunafanya kila linalowezekana ndani ya uwezo
wetu kujua ndege hiyo ilipo," Hishammuddin Hussein amewaambia waandishi
wa habari katika mji Kuala Lumpur.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment