
Australia inadadisi picha za Satelite za vitu viwili vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege iliyopotea ya Malaysia.
Nchi hio inashirikiana na Norway, New Zealand na Marekani kutafuta mabaki hayo.
Upepo mkali na mvua zilitatiza
juhudi hizo hii leo na kusababisha shughuli hiyo kusitishwa. Hata hivyo
msako huo utaendelea siku ya Ijumaa.

Picha za Satelite za kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott mapema leo
aliambia bunge la nchi hio kuwa picha zilizonaswa na mitambo ya Satelite
ya nchi hio baharini, zilionekana kama vipande viwili vya mabaki ya
ndege hiyo.
Kipande kimoja kilikuwa na urefu wa mita 24.
Bwana Tony Abbott,aliambia bunge kuwa hii ni taarifa mpya na iliyothibitishwa.
Lakini maafisa wakuu nchini Malaysia
wametahadharisha kuwa mabaki hayo huenda sio ya ndege yake, ambayo
ilipotea siku kumi na tatu zilizopita ikiwa imewabeba watu 239 kuelekea
Beijing.
Mabaki hayo yalionekana umbali wa kilomita elfu mbili miatano Kusini Magharibi mwa mji wa Perth.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment