Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema tatizo la
umaskini linalowakabili Watanzania, linatokana na viongozi walioko
madaraka kutokuwa waadilifu.
Alisema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali
nyingi ambazo kama zikisimamiwa vyema taifa haliwezi kuwa na watu
maskini kama ilivyo hivi sasa.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza
kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Vijiji vya Igula katika
Kata ya Luwota na Magulilwa mkoani Iringa.
“Nchi hii siyo maskini, imejaliwa rasilimali
nyingi ambazo kama zikisimamiwa ipaswavyo, taifa lisingekuwa na umaskini
kama ilivyo sasa,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Leo hii viongozi wa CCM wamekosa uadilifu ndiyo maana magogo kutoka katika misitu yetu yanaibiwa na kupelekwa nje ya nchi.
Dk Slaa alisema hayo yanatokana taifa kuongozwa na
watu wasio waadilifu, huku Amiri Jeshi Mkuu ambaye pia ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete akishindwa kukabiliana na hali hiyo.
Katika mikutano hiyo, Dk Slaa aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua mbunge wao ili kuongeza idadi ya wabunge wake.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Katika mikutano hiyo, Dk Slaa aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua mbunge wao ili kuongeza idadi ya wabunge wake.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment