ONESTORY
Mgaya (31) mkazi wa kijiji cha Madaba Wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma
anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Nesta
Mgaya mwenye umri wa miezi saba kwa kumbamiza chini kwenye barabara ya ltami.
Kamamnda
wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimenke amesema,tukio hilo
limetokea februari 9 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi eneo la kijiji
cha Lilondo wilayani humo.
Amesema, inadaiwa
siku ya tukio mtuhumiwa na mkewe Blesila Mponda (30) pamoja na mtoto
wao Nesta walifunga safari kutoka Madaba kwenda Lilondo kumsalimia mama
wa mtuhumiwa ambapo wakati wakiwa wanarudi nyumbani kwao wakiwa njiani
kutoka nyumbani kwao na mtuhumiwa wakielekea kituo cha mabasi Blesila
aligundua kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto
wao hivyo alilazimika kumwachia mtoto mtuhumiwa ili kwenda kuchukua
kadi hiyo.
Amesema,
mtuhumiwa akiwa amembeba mwanaye kuelekea kituoni ghafla alianza
kumbamiza huyo mtoto chini kwenye barabara ya lami akiwa amemshika
miguu na kumpigiza kichwa chini ambapo wakati akiendelea kufanya unyama
huo watu waliokuwa jirani walifika na kwenda kutoa msaada ambapo
mtuhumiwa alikimbilia porini na kumwacha mtoto chini.
Amefafanua
zaidi kuwa, inadaiwa wananchi walilazimika kumkibiza mtoto huyo kwenye
kituo cha afya cha Madaba na kutokana na kuumizwa vibaya kichwani
alihamishiwa hospitali ya serikali ya Rufaa Songea ambapo alilazwa wodi
ya majeruhi kwa matibabu na siku iliyofuata aliaga dunia.
Hata hivyo Kamanda Nsimenke ameeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa siku
hiyohiyo ya tukio na anatarajiwa kupelekwa kupimwa akili ili aweze kufunguliwa mashitaka.
Chanzo: Mtandao-net
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment