
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira, James Lembeli akiwasilisha taarifa kuhusu tathmini ya
matatizo yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili, bungeni Dodoma.
Wananchi mbalimbali wakiwamo wasomi na wabunge, wamelitaka Bunge
kuweka wazi majina ya wabunge waliotajwa kuhusika na vitendo vya
ujangili wa wanyamapori.
Wakati akiwasilisha taarifa ya Kamati ndogo ya
Uchunguzi ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni
Tokomeza Ujangili, Mwenyekiti wake, James Lembeli alisema baadhi ya
wabunge walitajwa kujihusisha na ujangili.
Akizungumza jana, Wakili wa siku nyingi nchini,
Peter Shayo alisema ili Serikali na Bunge waonekane wako makini na
wanachukizwa na vitendo vya ujangili ni lazima wawataje hadharani
wabunge hao.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter
Msigwa alisema jana kuwa hakuona mantiki ya kamati hiyo kutowataja
wabunge hao.
Mwanasayansi bingwa mtafiti, Profesa Watoky Nkya
alisema: “Kamati imetumia fedha nyingi za kodi za wananchi wakijua
hakuna aliye juu ya sheria. Tulitarajia kuwafahamu wote waliohusika na
ujangili.”
Diwani wa Kata ya Shighati, Enea Mrutu alisema
haiwezekani wabunge wawang’oe mawaziri wanne lakini miongoni mwao wapo
wanaotuhumiwa kwa ujangili na kuachwa bila kutajwa.
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alisema: “Kazi
yetu wabunge ni kuisimamia Serikali, kwa hiyo wale wabunge waliotajwa
watajwe ili nao wawajibike ili Bunge letu liwe na nia thabiti ya
kuisimamia Serikali,” alisema Mbatia.
Akizungumzia madai hayo, Lembeli alisema majina ya wabunge hao yapo kwenye viambatanisho vya ripoti yake kwa Bunge.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment