Thamsanqa Dyantyi mfasiri wa lugha za ishara anayelalamikiwa
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa
mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha
Nelson Mandela imekuwa ikidanganya kwa miaka mingi na imekuwa ikitoa
wafasiri wenye kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mfasiri
huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati
wa ibada hiyo siku ya jumanne.
Naibu Waziri wa Afrika Kusini
Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka
taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani
alikuwa na vibali halali.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mfasiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya
viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana
Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
"Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kilikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment