Julius Mtatiro
Lengo lao ni kutugawanya watutawale.

Wakuu,
Nimejulishwa pia kwamba waziri Lukuvi alisema uongo mwingine mkubwa, jana (juzi) tarehe 08 Nov 2013 bungeni, kwamba "kwenye mazungumzo ya vyama na serikali ati kuna wakati wajumbe wa vyama(TCD) walishindwa kuelewana na wakaomba faragha na ati wakapewa chumba maalum katika ofisi ya Waziri Mkuu na eti huko chumbani kuna wakati wajumbe wa vyama(TCD) walishindana kwa kupiga kura na wanne walikubaliana wawili wakakataa na eti yeye Lukuvi ana CD ya kikao hicho cha faragha"

UKWELI NI NINI.

Kama kweli Lukuvi kasema maneno hayo ni mwongo, tena mwongo wa ajabu kweli.

Mimi na Mnyika tuliongoza TC ya vyama, katika siku mbili za majadiliano haikuwahi kutokea tukaomba chumba ili tukubaliane jambo na wala hatukuwahi kwenda faragha na wala hakukuwahi kuwa na jambo tunalobishania sisi kwa sisi kwani hoja zilizotupeleka mezani tayari zilishapitishwa na viongozi wakuu wa vyama vyetu.

Mfumo tuliotumia ni kwamba, tulifanya majadiliano siku ya kwanza, siku nzima! na ilipofika jioni masuala ambayo hatukukubaliana tukasema kila upande urudi kwa wakubwa. Sie TC ya vyama tukaondoka hadi ofisi ya BUNGE chumba cha kiongozi wa kambi ya upinzani, tukapanga "modalities" za kutumia keshoye na mambo yapi tuwajulishe viongozi wakuu ili watushauri, kikao hiki cha ofisi za bunge hakikuwa na mvutano wowote na kilikuwa na mashauriano mazuri na hitimisho la kila jambo bila mvutano.

Kesho yake tulianza mazungumzo kama kawaida pale ofisi ya waziri Mkuu, pana mambo serikali ikalegeza msimamo na pana mambo wakasimamia wanayoyataka wao, tukakubaliana katika baadhi ya masuala na tukakubaliana kutokukubaliana kwa baadhi ya mengine, kikao kikafungwa, hii "day two" pia haikuwa na faragha yoyote ile tuliyokaa, iwe pale kwenye ukumbi wa mikutano au katika chumba.

Kama kweli Lukuvi kasema maneno hayo basi Tanzania ina kazi kubwa sana hadi kuifikia demokrasia ya kweli.

Julius S. Mtatiro - Johannesburg.
FB 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top