Kiongozi wa wapiganaji wa M23 mashariki mwa Jamhuri
ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita
vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba
anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili
kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.
Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha
kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni waliwasukuma nyuma
wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.
Mazungumzo ya amani yanafanyika mjini Kampala, Uganda.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment