Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi katika mji wa pwani wa Syria wa Latakia.
Hii ni kwa mujibu wa afisaa mkuu wa Marekani
ambaye alisema kuwa shambulizi hilo lililenga makombora ya Urusi yaliyokuwa
yananuiwa kupelekwa kundi la wapiganaji la Hezbollah.
Latakia ni ngome ya kisiasa ya Rais Bashar al-Assad, na pia kuwa mji muhimu ambako jamii yake ya Alawite inatoka.
Israel, inasemekana kufanya angalau mashambulizi matatu ya angani dhidi ya Syria mwaka huu pekee.
Taarifa hii inajiri huku kikundi cha wataalamu
wa silaha za kemikali kutoka shirika la OPCW waliokuwa na jukumu la
kuharibu vifaa vya silaha za kemikali vya Syria, kusema kuwa
limekamilisha kazi yake siku moja kabla ya makataa iliyotolewa.
Hatua ya shirika hilo ilitokana na makubaliano
yaliyofikiwa kufuatia madai yaliyokanushwa na serikali ya Syria kuwa
majeshi yake yalitumia nguvu pamoja na silaha za kemikali katika maeneo
ya raia , na pia baada ya Marekani na Ufaransa kutishia kutumia nguvu za
kijeshi dhidi ya Serikali ya Syria.
Afisa huyo alisema kuwa mashambulizi yalifanyika Jumatano na kuendelea hadi Alhamisi serikali za Syria na .Urisi bado hazijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Israel imekuwa ikisema kuwa itachukua hatua
ikihisi kuwa silaha za Syria, ziwe za kemikali au za kawaida
zinapelekewa wapiganaji katika eneo hilo hasa kundi la wapiganaji la
Hezbollah.
Chanzo: BBC Swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment