Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
kidemokrasi ya Congo, ameambia baraza la usalama la Umoja huo kuwa
makali ya kundi la waasi la M23 kama tisho la kijeshi yamekwisha
Martin Kobler alisema kuwa kundi hilo limeondoka
katika maeneo yao ya kivita mashariki kwa DRC, na kwamba sasa wako
katika eneo dogo karibu na mpaka wa Rwanda.
Eneo lingine la tano lililokuwa ngome ya waasi hao liliweza kudhibitiwa na jeshi la serikali siku ya Jumatatu.
Waasi hao wanasema kuwa wameondoka katika maeneo yao ya vita kwa muda.
Aidha bwana Kobler aliambia baraza al usalama kupitia kwa njia ya Skype kuwa kwa sasa ni kama kundi ilo limefika mwisho wake.
Aliongeza kwamba waasi wameondoka katika ngome yao moja kuu ya mlima Hehu karibu na mpaka wa Rwanda.
Baada ya mkutano huo, balozi wa Ufaransa Gerard
Araud alisema anatumai kutakuwa na mazungumzo sasa kati ya waasi hao na
serikali.
Alisema: ‘‘Bwana Kobler ametuarifu kuwa
wanashuhudia mwisho wa kundi la M23 kama tisho la kijeshi. Kwa hivyo
naona kama ni hatua nzuri na kwamba hata kulikuwa na makubaliano kuwa
sasa tushinikize mazungumzo kuanza tena mjini Kampala.’’
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23, mjini Kampala, yalisitishwa wiki jana.
Hali hata hivyo hali ilikuwa imetulia Mashariki mwa DRC kwa muda wa wiki moja.
Watu walionekana wakishangilia wakati wanajeshi walipoingia mji wa Rumangabo ambao ulikuwa umetekwa na waasi hao
Na sasa serikali inadhibiti hali mjini humo, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Julien Paluku.
‘‘Tumekuwa na mikutano miwili ili kujadili
tutakavyoimarisha hali ya wananchi...na tutatangaza kuanza tena kutolewa
kwa huduma za serikali katika muda wa masaa 24,’’ alisema Paluku.
Mji wa Rumangabo – ulio umbali wa kilomita 50
Kaskazini mwa Goma, mji rasmi wa Mashariki mwa DRC, ulikuwa na kambi
tatu kubwa za kijeshi nchini humo kabla ya kutekwa na waasi wa M23 mwaka
jana.
Hapana shaka kuwa majeshi ya serikali yamefikia hatua kubwa na kupata ushindi mkubwa dhidi ya waasi,
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment