Wakaazi wa Barawe wanasema walionda ndege ikipaa angani baada ya kurusha kombora kubwa.
Shambulizi la angani Kusini mwa Somalia dhidi ya
kundi la Al Shabaab limewaua viongozi wawili wa kundi hilo. Hii ni kwa
mujibu wa wenyeji wa mji wa Barawe.
Shambulizi hilo liliharibu gari la wanamgambo
hao waliokuwa wanasafiri kati ya miji ya Jilib na Barawe, inayoonekana
kuwa ngome ya kundi hilo.
Mapema mwezi huu Marekani ilifanya mashambulizi yaliyotibuka wakitaka kumkamata kamanda wa kundi hilo.
Al-Shabaab ni kundi rasmi linalohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda- Afrika Mashariki.
Duru za kijeshi nchini Kenya ziliambia BBC kuwa jeshi lao lilivamia mji wa Jilib, na huenda baadhi ya wanamgambo walijeruhiwa.
Hata hivyo, wadadisi wanasema kuwa huenda sio wanajeshi wa Kenya waliofanya mashambulizi ya angani.
Wakaazi wa mji wa Jilib, ulio umbali wa kilomita
120 Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Kismayo, waliambia BBC kuwa
huenda makomando hao wawili waliuawa kwa kutumia ndege zisizo na rubani.
Mmoja wa waliouawa alikuwa mtaalamu wa silaha wa
kundi hilo anayejulikana kama Anta, mmoja wa kundi hilo aliliambia shirika
la habari la AP.
Hii leo nilisikia mlipuko mkbwa na kuiona ndege
isiyo na rubani ikiishia angani, angalau makomanda wawili waliuawa,’’
alisema mkaazi mmoja wa eneo hilo kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters.
"Niliona gari likiteketea na wanaume wengi wa Al
Shabaab walikuja katika eneo hilo. Na pia niliwaona wakibeba maiti za
wawili hao.’’
''Ndege hiyo ilirusha kombora kubwa na magari mengi yalikuwa mbele yangu ingawa ni gari la magaidi hao lililoshambuliwa tu.''
Angalau watu 67 waliuawa mwezi jana wakati kundi la Al shabaab liliposhambulia jengo la Westgate mjini Nairobi.
Makomando wa Marekani walivamia mji wa Barawe
baada ya shambulizi la Nairobi, ingawa walilazimika kuondoka baada ya
mashambulizi yao kutibuka.
Makomando hao walitaka kumkamata kamanda mmoja
mkuu wa kundi hilo Abdukadir Mohamed Abdukadir, anayejulikana kwa jina
lingine kaka Ikrima.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment