Mo
Wakfu wa Mo Ibrahim ambao humzawidia Rais mstaafu
aliyeonyesha uongozi mzuri umesema hakuna kiongozi wa Afrika aliyetosha
kutuzwa mwaka huu.
Hata hivyo utafiti wa wakfu wa Mo umeonyesha
kuwa Afrika imepiga hatua pakubwa tangu mwanzoni mwa karne hii katika
maswala ya uongozi.
Tuzo hiyo haijapata mshindi kwa miaka minne mfululizo tangu kuzinduliwa kwake miaka saba iliyopita.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini
London, wakfu wa Mo umesema kuwa baada ya ukaguzi kufanyika hakuna hata
kiongozi mmoja alistahili kutuzwa.
Tuzo hiyo ambayo hutolewa na mfanyabiashara
bilionea mzaliwa wa Sudan na raia wa Uingereza, Mo Ibrahim hutoa dola
milioni 5 kwa kipindi cha miaka kumi na dola laki mbili kila mwaka hadi
kiongozi huyo atakapofariki. Na pia dola laki zingine mbili hutolewa kwa
mradi wowote unaoungwa mkono na mshindi wa tuzo hiyo kwa kipindi cha
miaka kumi.
Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu za wakfu huo, kuna baadhi ya sehemu ambapo hali bado ni mbaya ikiwemo kutii sheria.
Wakfu huo wake Mo Ibrahim tajiri mkubwa sana
mwenye uraia wa Sudan ulianza kutoa takwimu zake kuhusu utawala barani
Afrika mwaka 2007.
Katika mwaka ambapo Afrika ilisherehekea miaka
hamsini tangu kuzinduliwa kwa muungano wa nchi za Afrika, AU ambapo kwa mujibu
wa utafiti wa wakfu wa Mo Ibrahim, mustakabali wa Afrika sio mbaya.
Washindi wa tuzo ya Mo
2005 Joaquim Chissano: Msumbiji
2008 Festus Mogae : Botswana
2011 Pedro Pires : Cape Verde
2008 Festus Mogae : Botswana
2011 Pedro Pires : Cape Verde
Asilimia tisini na nne ya waafrika sasa wanaishi katika nchi ambayo angalau imeonyesha uongozi umeimarika tangu mwaka 2000.
Nchi 18 kati ya hamsini na mbili, zilionekana kupata alama nzuri tangu mwaka 2007.
Utafiti huu unaanganzia mambo kadha kwa kadha kama vigezo vya utawala mzuri ikiwemo, ukuwaji wa uchumi , afya na sheria.
Taifa lililopata alam,a nzuri kuliko zote ni Mauritius,ikifuatiwa na Botswana na Cape Verde.
Mataifa yaliyoshika mkia ni pamoja na Eritrea,
DRC na Somalia. Nchi zenye uchumi mkubwa barani Afrika,ikiwemo Afrika
Kusini na Nigeria zilishika nambariya sita na 45 mtawalia.
Ripoti ya Mo inaonyesha kuwa mizozo sasa imepungua barani humo kuliko ilivyokuwa mwongo mmoja uliopita.
Hata hivyo, bado kuna tatizo la pengo kubwa kati
ya masikini na matajiri na ripoti hiyo inaonya kuwa ikiwa tatizo hili
litapuuzwa huenda mizozo zaidi ikaibuka.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment