Mitaala ya Elimu katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu imewekwa katika tovuti hii.

Mitaala hii ni ile iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2005 ambayo ilizingatia ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana badala ya ule wa awali unaozingatia maarifa. Mitaala hii imekuwa ikitumika kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2005 hadi hivi sasa.

Mitaala imeboreshwa kufuatia mchakato wa majadiliano katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyofanyika mwezi Februari 2013, pamoja na maoni na hoja mbalimbali zilizotoka kwa wadau wa elimu.

Pamoja na maboresho yaliyofanyika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweka mitaala hii wazi kwa wadau wote wa elimu na jamii kwa ujumla ili kuendelea kupata maoni zaidi ya jinsi na namna ya kuiboresha mitaala hiyo.

Aidha, katika kipindi hiki cha kukusanya maoni, mitaala hii itaendelea kutumika hadi hapo mchakato wa kuihuisha utakapokuwa umekamilika.

icon MTAALA WA ELIMU YA AWALI (90.51 kB)
icon MTAALA WA ELIMU YA MSINGI (129.81 kB)
icon CURRICULUM FOR ORDINARY LEVEL SECONDARY EDUCATION (184.15 kB)
icon CURRICULUM FOR ADVANCED SECONDARY EDUCATION (240.27 kB)
icon CURRICULUM FOR CERTIFICATE IN TEACHER EDUCATION (332.33 kB)
icon CURRICULUM FOR DIPLOMA IN TEACHER EDUCATION (192.09 kB)

Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top