Maandamano na mikutano ya hadhara iliyokuwa imeandaliwa na vyama vya NCCR, CHADEMA na CUF katika maeneo ya Unguja, Dar, Arusha, Mwanza, Tanga, Mbeya, Dodoma na Kigoma na kupaswa kufanyika siku ya alhamisi 10.10.2013, imeahirishwa hadi mtakavyojulishwa vinginevyo.

Sababu ya kuahirisha ni kutoa fursa kwa mazungumzo kati ya vyama na Rais baada ya maombi ya Serikali. Ikiwa mazungumzo hayatazaa matunda na ikiwa hoja za kulinda maslahi ya umma katika mchakato wa katiba hazitazingatiwa, ratiba ya maandamano na mikutano itatangazwa upya na kufanyika bila kipingamizi.

Viongozi wakuu wa vyama wameongea na vyombo vya habari leo hii makao makuu ya NCCR. Tusubiri tuone nini hatma ya mazungumzo.

J. Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Ushirikiano wa Vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA.
Fb 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top