Maafisa wa India wanaoshughulika na kazi za uokozi
wameanza shughuli zao baada ya Kimbunga Phailin kupiga majimbo ya
mashariki na kusababisha mafuriko kwenye miji na vijiji.
Wakuu wanasema wasaidizi wametumwa maeneo
yaliyopigwa na kimbunga katika majimbo ya Orissa na Andhra Pardesh,
kuwaokoa wale wanaofikiriwa wamenasa chini ya vifusi.
Miti iliyoporomoka imeua watu wapatao saba ingawa waandishi wa habari wanasema matayarisho
na operesheni kubwa iliyofanywa ya kuwahamisha watu kabla ya kimbunga,
imenusuru maisha ya watu.
Kiwango cha uharibifu uliotokea bado hakijulikani kikamilifu ingawa waya za umeme na mawasiliano vimekatika katika maeneo mengi.
Kimbunga cha mwaka 1999 kiliuwa watu 10,000 katika jimbo la Orissa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment